Maandalizi ya bwawa la samaki ni hatua muhimu sana katika mafanikio makubwa ya ufugaji samaki,bwawa la samaki likiandaliwa ipasavyo na kufuata utaratibu mzuri hua ni chanzo cha mafanikio katika ufugaji samaki,lakini wafugaji wengi wasamaki huanguka na kupata hasara kubwa na mafanikio madogo ya ufugaji samaki sababu ya kukosa elimu ya kuandaa bwawa la samaki vizuri kama inavyotakiwa.zifuatazo ni hatua muhimu za kuandaa bwawa la samaki kabla ya kuwaweka ndani ya bwawa.
Tengeneza bwawa lako katika eneo lisilokua na mteremko mkali,eneo lenye maji yakutosha,eneo lenye udongo mfinyanzi na eneo lililo mbali na uchafuzi wa majitaka.
Jaza maji safi na salama ndani ya bwawa,usijaribu kuweka maji yenye chlorine ndani ya bwawa.
Weka mbolea ya kuku au ya mfugo wowote kwenye bwawa,weka kilo tatu kwa kila mita mia moja za eneo la bwawa lako (5kg/100m2)
Baada ya kuweka mbolea subiri wiki mbili kabla ya kuweka samaki ndani ya bwawa ili chakula asilia cha samaki kuota ndani ya bwawa.(ukijani wa maji na vijidudu vidogo).
Weka samaki ndani ya bwawa kulingana na ukubwa wa bwawa,weka vifaranga watano hadi kumi wa kambare kwa kila mita moja za eneo la bwawa(5-10kambare/m2)
JINSI YA KUWEKA MBOLEA KWENYE BWAWA LA SAMAKI KWAAJILI YA KURUTUBISHA BWAWA.
Kurutubisha bwawa ni kuongeza mbolea asilia au ya kiwandani katika bwawa kwaajili ya kurutubisha bwawa na kuzalisha chakula asilia cha samaki ambacho nichanzo kizuri sana cha chakula kwa samaki,mfano wa chakula asilia ni kama vimajani vidogovidogo na wadudu wadogowadogo (phytoplankton na zooplankton).
4.1. MUDA AMBAO HAUHITAJIKI KUWEKA MBOLEA KATIKA BWAWA
Muda wa usiku
Wakati joto la maji ya bwawa limeshuka
Wakati wa baridi
Wakati wa mawingu pasipokuwa na mwanga wa jua
Wakati maji ya bwawa yana rangi ya kijani iliyo zidi.
Ukiweka mbolea pasipo kufuata utaratibu itapelekea kupungua kwa hewa ya oxygen ndani ya bwawa na kusababisha kufa kwa samaki, vilevile mbolea ikizidi husababisha maji kuchafuka na kuota kwa kukithiri kwa chakula cha samaki ambapo hufunika uso wa maji ya bwawa na kuzuia kuingia kwa hewa ya oxygen ndani ya bwawa la samaki.
4.2. MUDA SAHIHI WA KUWEKA MBOLEA KWEMYE BWAWA LA SAMAKI
Wakati mwanga wa jua umetoka
Wakati hakuna mawingu
Maji ya bwawa yakiwa yanajoto
Wakati maji hayana rangi ya kijani ya kutosha
4.3. KIWANGO SAHIHI CHA KUWEKA MBOLEA KATIKA BWAWA LA SAMAKI
Unaweza kutumia mbolea ya kuku,ng’ombe,farasi,nguruwe na mifungo yote au mbolea yeyote inayo tokana na wanyama au ukatumia mbolea za viwandani,ila mbolea ya kuku ni bora zaidi kuliko mbolea zote za mifugo.
Tumia kilo 2 hadi 3 za mbolea ya kuku kwa kila mita 100 za eneo la bwawa la samaki kwa kila wiki
Tumia kilo 8 hadi 10 za mbolea ya nguruwe kwa kila mita 100 za eneo la bwawa kwa kila wiki
Tumia kilo 10 hadi 15 za mbolea ya ng’ombe kwa kila mita 100 za eneo la bwawa la samaki kwa kila wiki
Au unaweza kutumia kilo 6 hadi 20 za mchanganyiko wa mbolea zote za mifugo kwa kila mita 100 za eneo la bwawa la samaki kwa kila wiki.
Tumia kilo 0.4 hadi 0.8 za mbolea ya nitrogen kwa kila mita 100 za eneo la bwawa la samaki
Tumia liko 0.1 hadi 0.2 za mbolea ya phosphorous kwa kila mita 100 za eneo la bwawa la samaki.
ONYO. Kuzidisha mbolea kwenye bwawa la samaki ni hatari sana katika maisha ya samaki ndani ya bwawa,hii ni sababu mbolea ikizidi kwenye bwawa husababisha kupungua kwa hewa ya oxygen ndani ya bwawa na husababisha kuota kwa algae nyingi ndani ya bwawa na maji kuchafuka na kusababisha samaki kufa na kutokukua vizuri kama inavyotakiwa,pia husabaisha mlipuko wa magojwa hatari kwa samaki.
4.4. JNSI YA KUWEKA MBOLEA KATKA BWAWA LA SAMAKI
Kuna njia mbalimbali za kuweka mbolea kwenye bwawa la samaki zifuatazo ni baadhi ya njia muhimu zinazotumika zaidi.
Tengeneza kiukuta kidogo kwenye kona ya bwawa la samaki kwa kutumia nguzo ndogondogo za miti,kisha weka mbolea ndani ya ukuta na kuhakikisha kuwa mbomea haipenyezi na kuingia au kusambaa ndani ya bwawa la samaki
Njia ya pili ya kuweka mbolea kwenye bwawa ,chuku gunia au mfuko wa salifeti au magunia ya kuhifadhia mahindi kisha jaza mbole ndani ya gunia baada ya kujaza funga vizuri na toboa vitundu vidogovidogo kila sehemu ya gunia kisha tumbukiza ndani ya bwawa na ulifunge na kamba ililisitembee ndani ya bwawa,