Jumanne, 1 Januari 2019

Jinsi ya kuuza samaki wako kidijitari

JINSI YA KUUZA SAMAKI BWAWANI KWAKO. 
Wafugaji wengi hutegemea kuuza samiki wote kwa jumla kitu amabacho kinawezekana ila kwa uchache sana . Sasa ukikosa wanunuaji wa jumla unafanyeje? Wengi hukaa na samaki bila kujiongeza na kumbuka wanavyo kaa bwawani gharama inaongezeka maana jinsi wanavyokua wakubwa ndio uhitaji wa chakula unaongezeka na maji huchafuka haraka kutokana na wingi wa taka mwili hivyo utarazimika kubadilisha maji mara kwa mara.
 Fanya hivi
Tafuta wateja kabla samaki hawajafikia muda wa kuvunwa lakini mpango "B" Tengeneza CAGE(hapa) ni wavu kinachofungia samaki ndani ya bwawa kubwa ili kuwe na urahisi wakuwatoa muda wowote ukiwahitaji. Mfano wa Fish cage ni net ya mmbu , nyavu za madilisha hata waya mesh
Faida za cage

  • Inakusaidia kuuza samaki hata kuanzia kg 1 mteje anapopatikana
  • Inapunguza  gharama ya uvunaji maana bila cage kama bwawa ni kubwa utarazimika kutoa maji kila unapohitaji samaki lakini unapokuwa na cage unavua mara 1 unawaweka kwa cage . 
  • Pia wakiwa kwa cage unaweza kupandikiza vifaranga wengine


  • Hasara za cage Kama hakuna ulinzi ni rahisi kuondoka na samaki kama utatengeneza cage rahisi na bila ushauri. 


Tunauza vifaranga 
Kambale 300
Sato 350 
0718593224
0715926398whatup(BAGAMOYO)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni