TUNAKODISHA NA KUSIMAMIA HATUA ZOTE HADI SOKONI.
Hali ya hewa.
Kitunguu hustawi katika hali ya hewa ya nyuzi 15°c hadi 28°c . Hivyo Bagamoyo inafaa.
Aina za vituguu.
Kwa Tanzania tunalima vitunguu vya aina 3
- Red creole
- Red Bombay na
- Texas Grano
Kusiha mbegu kwa kitaru.
Kilo 2 zinatoa miche ya heka 1
Kitaru kinatakiwa kuandaliwa kwa leki ili kulainisha udongo au kutumia majivu au sehemu palipochomwa mkaa maana udongo ule hakunaga wadudu. Mistari iwe na urefu wa 1cm kwenda chini , mwaga mbegu polepole fukia kwa udongo laini. Kwa Bonde ruvu mbegu zitachukua siku 4 hadi 10 kwa sababu ya joto kwa maeneo mengine huchukua hadi siku 20. Ni muhimu kumwagilia maji ya kutosha kwa siku 10 za mwanzo. Miche ikae mwezi1 kwa kitaru ihamishiwe shambani ikiwa na upana wa penseli na urefu wa 15 cm.
Kupanda miche kwa jaruba
Tunatumia jaruba la 5m kwa 3m au zaidi. Miche hupandwa kwa nafasi ya upana wa 20 cm na nafasi ya 10 cm kati ya mistari.
Mbolea.
Tunatumia mbolea za NPK heka inahitaji kg 200 na huwekwa siku 7 kabla ya kupanda kisha inashauriwa kuweka mbolea ya nitrogen ili kunenepesha kg 13 huwekwa wiki3 hadi 4bkupanda
kupanda . kiasi 10gm /1m2
Umwagiliaji.
Maji yanatakiwa kulowanisha udongo kwa 1cm kwenda chini au zaidi mwagilia kila baada ya wiki 1 hakikisha maji hayatuami maana yatasababisha ugonjwa wa kuoza kwa bulb.
Mavuno.
Kwa Bagamoyo heka hutoa gunia 120 bei ya shambani ni laki na kumi mwezi wa 6 mpaka wa 10 lakini hupanda zaidi miezi ya mvua kukiwa kuna shida ya usafiri wa kwenda kuchukua mazao mikoani.
Soko la vitunguu.
Soko ni kubwa la ndani na nje na ukiona soko halilizishi tunakupa eneo la muhifadhia magunia yako mpaka soko liwe zuri aidha tuna uzoefu wa masoko wa miaka 14 ya ndani na nje.
Gharama kwa heka 1
Kukodi miezi 6...................................... 300, 000
Kulima trekta............................................ 70, 000
Halo..............................................................50, 000
Jaruba .......................................................200, 000
Kupanda................................................... 20, 000
Mbegu kg 3@ mtaan 70000 hybrid....150, 000
Kupalilix2 .................................................240, 000
Dawa.......................................................... 100, 000
Mbolea kg 200 NPK , 18 NITROGEN .. 250, 000
Mashine ya kumwagilia....................... 350, 000
NB:Gharama inaweza Badilika
Aidha tunakodisha mashine za umwagiliaji kwa wasionazo
Pia tunasimamia kwa mazao yote kama tikiti , nyanya , hoho, mahindi mabichi na mpunga n. K.
Tupo kituo cha daladala kiitwacho Mtoni njia ya kiwangwa ukitoke Bagamoyo ni km 7
Kwa michanganuo inayosadifu uhalisia tembelea
Shambalink. blogspot. Com
0715926398
Karibu sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni